Jinsi ya Kupata Barua Pepe ya Kampuni (info@biasharayako.co.tz)
Print- barua pepe ya kampuni, email ya biashara, business email kiswahili, email co.tz
- 0
Barua pepe ya kampuni kama info@biasharayako.co.tz inaifanya biashara yako ionekane halali na ya kuaminika kuliko kutumia anwani za bure kama Gmail. Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kupata barua pepe ya kampuni Tanzania.
Kwa nini barua pepe ya kampuni ni muhimu?
- Uaminifu – wateja, benki na kamati za zabuni huziamini zaidi.
- Umiliki – mfanyakazi akiondoka, barua pepe na kumbukumbu zinabaki kwa kampuni.
- Utambulisho – kila barua pepe unayotuma inatangaza jina na tovuti yako.
Unachohitaji
- Domain – kwa mfano biasharayako.co.tz (TZS 25,000 kwa mwaka). Sajili hapa.
- Huduma ya barua pepe – kila kifurushi cha hosting kina barua pepe bila kikomo, au chagua kifurushi cha barua pepe pekee kuanzia TZS 55,000 kwa mwaka.
Hatua za kuanza
- Chagua na usajili domain yako.
- Agiza hosting au kifurushi cha barua pepe na ulipe kwa M-PESA, Mixx by YAS, Airtel Money au kadi.
- Tengeneza anwani kama info@, sales@ na majina ya wafanyakazi.
- Weka barua pepe kwenye simu yako. Soma mwongozo wa kuweka barua pepe kwenye simu (Kiingereza).
Je, naweza kutumia app ya Gmail?
Ndiyo. Unaweza kusoma na kutuma barua pepe za kampuni kupitia app ya Gmail kwenye Android au iPhone.
Unahitaji msaada wa kuanza? Timu yetu itakusaidia kuweka kila kitu. Tuandikie WhatsApp au angalia vifurushi vya barua pepe.