Jinsi ya Kutengeneza Tovuti ya Biashara Tanzania: Mwongozo Kamili
Print
  • kutengeneza tovuti, tovuti ya biashara, website tanzania, bei ya tovuti
  • 0

Tovuti ni ofisi ya biashara yako mtandaoni inayofanya kazi saa 24. Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kutengeneza tovuti ya biashara Tanzania hatua kwa hatua.

Hatua ya 1: Chagua jina la domain

Domain ni anwani ya tovuti yako, kwa mfano biasharayako.co.tz. Chagua jina fupi, rahisi kukumbuka na linalofanana na jina la biashara yako. Domain ya .co.tz ni TZS 25,000 kwa mwaka. Angalia usajili wa domain.

Hatua ya 2: Pata hosting

Hosting ni mahali tovuti yako inapohifadhiwa ili ionekane mtandaoni. Vifurushi vyetu vinaanzia TZS 50,000 kwa mwaka, vikiwa na SSL bure, backup kila siku na barua pepe bila kikomo. Angalia huduma za hosting.

Hatua ya 3: Panga kurasa za tovuti

  • Mwanzo (Home) – muhtasari wa biashara na huduma zako.
  • Kuhusu Sisi – historia, timu na sababu za kukuchagua.
  • Huduma au Bidhaa – ukurasa kwa kila huduma kuu.
  • Mawasiliano – simu, WhatsApp, barua pepe, anwani na ramani.

Hatua ya 4: Jenga tovuti

Unaweza kutumia WordPress ukiwa na ujuzi kidogo, au kuajiri wataalamu wakutengenezee. Tovuti nzuri inafunguka haraka kwenye simu, ina picha halisi na maelezo yaliyo wazi.

Hatua ya 5: Weka barua pepe za kampuni

Tengeneza barua pepe kama info@biasharayako.co.tz ili uonekane wa kitaalamu kwa wateja.

Hatua ya 6: Ifanye ionekane Google

Fungua Google Business Profile, tumia maneno ambayo wateja wanayatafuta, na omba maoni ya wateja. Soma mwongozo wetu wa SEO kwa Kiswahili.

Gharama ya tovuti

Gharama inategemea idadi ya kurasa na huduma unazohitaji, kama duka la mtandaoni au malipo kwa M-PESA. Soma pia gharama za kutengeneza tovuti (Kiingereza).

Unataka tukutengenezee tovuti? Tuandikie WhatsApp au angalia huduma zetu za kutengeneza tovuti.

Was this answer helpful?

Related Articles